Lugha Nyingine
Ustawishaji wa sekta ya usambazaji wa vifurushi ya China waonyesha soko la watumiaji linalokua
Muonyeshaji bidhaa akiandaa gari linalojiendesha kiotomatiki la kubeba na kuwasilisha vifurushi linaloonyeshwa kwenye Maonyesho ya Teknolojia za Kisasa ya Dunia Mwaka 2024 mjini Tianjin, Kaskazini mwa China, Juni 20, 2024. (Xinhua/Sun Fanyue)
BEIJING - Sekta ya usambazaji wa vifurushi ya China imevuka alama ya kusafirisha vifurushi bilioni 100 mwaka huu haraka zaidi kuliko mwaka uliopita, ikionyesha soko la wateja linalokua kwa kasi na ustawi endelevu wa kiuchumi.
Idadi hiyo ya vifurushi iliyofikiwa Jumanne, ni siku 71 mapema kuliko mwaka 2023, kwa mujibu wa Shirika la Posta la China (SPB). Hii ni sawa na wastani wa vifurushi 71.43 kwa kila mtu nchini China, au vifurushi 5,144 vinavyowasilishwa kwa wateja kila sekunde.
Sekta ya usambazaji wa vifurushi imekuwa kiashiria muhimu cha uchumi wa China. Huku kukiwa na uimarikaji thabiti wa uchumi, sekta hiyo imeweka rekodi mpya katika vipimo vitatu vikuu.
Kiwango cha juu zaidi cha usambazaji wa vifurushi kwa siku moja kilizidi vifurushi milioni 580, na wastani wa kila mwezi ulizidi vifurushi bilioni 13. Mapato ya kila mwezi ya sekta hii yalizidi Yuan bilioni 100 (dola karibu bilioni 14 za Kimarekani).
China inajivunia mtandao wa uchukuzi wenye ufanisi mkubwa ambao unafika hata maeneo ya mbali zaidi, ukiwa na vituo 234,000 vya usambazaji wa vifurushi nchini kote huku vijiji zaidi ya asilimia 95 vikiwa vimefikiwa na huduma hiyo. Msimu huu wa majira ya joto, mfumo huo umewezesha matunda ya msimu kutoka mikoa ya mbali kufikia wateja siku inayofuata.
Uvumbuzi wa teknolojia umeongeza zaidi ufanisi wa usambazaji wa vifurushi. Katika baadhi ya miji, droni zinaweza kusambaza vifurushi kwa muda wa dakika 10, wakati magari yanayojiendesha pia yamepunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kusambaza vifurushi.
China imekukwa ikiongoza duniani kwa huduma hiyo ya usambazaji wa vifurushi kwa miaka 10 mfululizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma