超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

China yatoa wito tena kulinda usalama wa njia ya meli katika Bahari Nyekundu

(CRI Online) Agosti 16, 2024

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang ametoa wito tena kwa kundi la Houthi la Yemen kuheshimu haki za usafiri wa meli za biashara za nchi mbalimbali kwa kufuata sheria za kimataifa katika eneo la Bahari Nyekundu, kuacha vitendo vya usumbufu, na kulinda usalama wa njia ya meli katika eneo hilo.

Balozi Geng amesema, China inakaribisha makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya serikali ya Yemen na kundi la Houthi kuhusu masuala ya fedha na usafiri wa anga, pia inatarajia kuwa pande zote zinazohusika zitaendelea na juhudi kama hizo na kumaliza migogoro kwa njia ya mazungumzo.

Pia amesisitiza kuwa China inatoa wito kwa pande zote zinazohusika kujizuia na kuacha vitendo vya kuongeza hali ya wasiwasi kaitka eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha