Lugha Nyingine
Sekta ya uzalishaji wa Mpira wa Hariri yastawishwa?huko Jingxi, Mkoa wa Guangxi, China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 28, 2024
Wakazi wakitengeneza mpira wa hariri katika Mtaa wa Jiuzhou, Kijiji cha Xinjing, Mji wa Jingxi, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Agosti 27. (Xinhua/Lu Boan) |
Katika miaka ya hivi karibuni, mpira wa hariri unaozalishwa huko Jingxi, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi umeuzwa nchini kote kama zawadi ya kupendeza na vitu vya kumbukumbu kwa watalii na marafiki. Pia umeuzwa katika Asia Kusini-Mashariki na maeneo mengine kupitia majukwaa ya biashara ya mtandaoni na uzalishaji wa mpira huo umekuwa sekta nzuri inayowezesha kukuza maendeleo ya utamaduni na utalii wa sehemu hiyo na kuongeza mapato ya wenyeji.
Mji wa Jingxi unajulikana kama "Mji wa Mpira wa Hariri wa China". Mpira wa hariri unaozalishwa huko unapendeza sana, na michora mbalimbali inatariziwa juu ya mpira. Ndani yake inaweza kujazwa na viungo au dawa ya mitishamba ya Kichina, ambayo imeonyesha sifa ya kipekee ya kikabila.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma