Lugha Nyingine
Mwalimu aleta matumaini kwa watoto katika sehemu za milimani za China (6)
GUIYANG - Meng Rongda mwenye umri wa miaka 59, ni mwalimu pekee wa "shule ndogo," kusema kwa usahihi zaidi ni mwalimu pekee wa kituo hicho cha mafunzo cha Mji Mdogo wa Xishan wa Wilaya ya Congjiang, Mkoa wa Guizhou, kusini-magharibi mwa China. Kwa sasa, kuna wanafunzi 23 wa shule ya awali na wanafunzi 17 katika darasa la kwanza na la pili la elimu ya msingi.
Mbali na Lugha ya Kichina na hesabu, Meng pia anawajibika kwa elimu ya michezo (PE) na mafunzo ya muziki ili kuhakikisha watoto wa vijijini wanaweza pia kupata elimu bora ya msingi.
Meng amekuwa akifanya kazi kama mwalimu, mpishi na mlezi katika shule hiyo ndogo tangu Mwaka 2015 katika sehemu ya milimani ambayo si rahisi kufikia huko. Kwake yeye, elimu inaweza kubadilisha hatma ya watoto na kwa hivyo, anajitolea kuangaza njia ya mbele kwa watoto hawa wa vijijini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma