Lugha Nyingine
Mkutano wa Kuwasiliana na Kufundishana kwa Utamaduni wa Kilimo wa “Mazungumzo na Dunia kuhusu Mashamba ya Ngazi ya Ziquejie” wafanyika (3)
Tarehe 12, Septemba, ufunguzi wa Mkutano wa pili wa Kuwasiliana na Kufundishana kwa Utamaduni wa Kilimo uitwao “Mazungumzo na Dunia Kuhusu Mashamba ya Ngazi ya Ziquejie” na mihadhara umefanyika katika Wilaya ya Xinhua ya Loudi, Mkoa wa Hunan China.
Kwenye ufunguzi huo wa mkutano yametolewa kwa "Makubaliano kuhusu Maendeleo ya Pamoja ya Kilimo, Utamaduni na Utalii Kwenye Mashamba ya Ngazi Duniani", makubaliano hayo yakieneza maoni mamoja kuhusu kuelewa ipasavyo thamani ya mashamba ya ngazi, kulinda mazingira ya asili ya mashamba ya ngazi, kurithisha utamaduni wa kilimo cha mashamba ya ngazi n.k.
Kwenye jukwaa la mihadhara lililofanyika baadaye, wajumbe kutoka nyanja za mali ya urithi wa utamaduni wa kilimo, na sekta za utamaduni na utalii walijadiliana kwa kina kuhusu namna ya kufanya vizuri ushirikiano na kufundishana katika nyanja ya utamaduni wa kilimo, kuhimiza uvumbuzi wa mafungamano ya kilimo, utamaduni na utalii, na kutia uhai mpya kwenye ustawishaji wa vijiji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma