Lugha Nyingine
Kampuni ya Afristar na Chuo Kikuu cha Nairobi waandaa kwa pamoja shughuli za kusherehekea Sikukuu ya Jadi ya Mbalamwezi ya China (6)
Afristar, kampuni ya kuendesha Kenya SGR na Chuo cha Confucius cha Chuo Kikuu cha Nairobi Ijumaa wamefanya kwa pamoja shughuli za kukaribisha Sikukuu ya Jadi ya Mbalamwezi, ambayo ni moja ya sikukuu muhimu zaidi za jadi za China na itakuwa Jumanne wiki ijayo kwa mwaka huu.
Shughuli hizo zilivutia watu zaidi ya 200, na zilikuwa pamoja na kucheza muziki za kijadi za China, kucheza dansi, kufanya maonyesho ya opera na mashairi, kupika keki za mwezi n.k.
Mwalimu wa Chuo cha Confucius cha Chuo Kikuu hicho Wang Xinyu alisema, shughuli hizo zilifanywa ili kuhimiza mawasiliano ya utamaduni kati ya nchi hizo mbili. “Kupitia kusherehekea pamoja sikukuu ya jadi, watu wa China na Kenya wanaelewana zaidi.”
Sikukuu ya Jadi ya Mbalamwezi ya China husherehekewa kila ifikapo tarehe 15 wa mwezi wa nane kwa kalenda ya jadi ya China. Sikukuu hiyo huwa wakati wa kujumuika kwa familia, kula pamoja keki za mwezi na kutazama mwezi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma