Lugha Nyingine
China yashuhudia safari za watalii milioni 765 wa ndani katika likizo ya siku 7 ya Siku ya Taifa
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 09, 2024
Watu wakitembelea mtaa wa kihistoria na kitamaduni katika Wilaya ya Xixiu ya Mji wa Anshun, Mkoani Guizhou, kusini-magharibi mwa China, Oktoba 2, 2024. (Picha na Chen Xi/Xinhua) |
BEIJING – Idadi ya watalii wa ndani wa China imefikia milioni 765 katika likizo ya siku 7 ya Siku ya Taifa iliyomalizika Jumatatu wiki hii, ikiwakilisha ongezeko la asilimia 5.9 kuliko mwaka jana wakati kama huo, takwimu kutoka Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China zimeonyesha.
Idadi hiyo ni asilimia 10.2 zaidi ya ile ya kipindi kama hicho Mwaka 2019, wizara hiyo imesema.
Thamani ya jumla ya matumizi katika manunuzi ya watalii hao wa ndani imezidi yuan bilioni 700 (dola za kimarekani kama bilioni 99.3) katika kipindi hicho, ikiongezeka kwa asilimia 6.3 kuliko mwaka jana na asilimia 7.9 ikilinganishwa na Mwaka 2019, kwa mujibu wa wizara hiyo.?
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma