超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yafanya mazishi ya waliokufamaji?kwenye?ajali?ya feri?iliyotokea?hivi karibuni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2024
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yafanya mazishi ya waliokufamaji?kwenye?ajali?ya feri?iliyotokea?hivi karibuni
Watu wakihudhuria mazishi ya watu waliokufamaji kwenye ajali ya hivi karibuni ya feri mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Oktoba 10, 2024. (Picha na Zanem Nety Zaidi/Xinhua)

GOMA, DR Congo - Mazishi rasmi yamefanyika jana Alhamisi mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kuwakumbuka watu waliokufamaji kwenye ajali mbaya ya feri iliyotokea hivi karibuni katika Ziwa Kivu.

Mazishi ya miili 11 iliyotambuliwa ya wakazi wa Goma waliofariki baada ya feri ya "MV MERDI" kupinduka katika Ziwa Kivu wiki moja iliyopita yamefanyika kwenye makaburi ya Makao. Watu takriban 87 walifariki Alhamisi wiki iliyopita baada ya feri hiyo kupinduka karibu na bandari ya Kituku, kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya jimbo hilo ambayo haikutaja idadi ya watu waliokuwemo.

Feri hiyo ilivunjika vipande vitatu na kwa sasa kiko kwenye kina kirefu cha mita takriban 198 katika Ziwa Kivu, amesema Makamu wa Gavana wa jimbo hilo Jean Romuald Lipopo ambaye alikuwepo kwenye mazishi hayo, akibainisha kuwa gesi ya methane katika Ziwa Kivu imekwamisha juhudi za msako.

Feri hiyo iliyokukwa ikitoka Minova katika Jimbo la Kivu Kusini, ilizama kwenye umbali wa mamia ya mita kutoka bandarini baada ya kushindwa kustahimili kasi ya wimbi kubwa, vyanzo vya habari katika bandari ya Kituku vimeeleza. Vyanzo hivyo vya eneo hilo vimeripoti kuwa feri hiyo ilibeba "mzigo mkubwa kupita kisai”.

Njia ya nchi kavu kati ya Goma na Minova imekatika kwa miezi kadhaa kutokana na uhasama kati ya makundi yenye silaha na wanajeshi wa DRC. Matukio ya ajali za meli zilirekodiwa mara kwa mara kwenye Ziwa Kivu kutokana na upepo mkali na kubeba mizigo kupita kiasi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha