Lugha Nyingine
Ujenzi wa Daraja la Juu zaidi duniani waingia kipindi kipya
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2024
Wafanyakazi wa shirika la daraja la Kundi la Ujenzi na Mawasiliano la Guizhou, China wakifanya maandalizi ya kufunga boriti ya kwanza ya chuma ya daraja. (Picha ilipigwa Novemba 4) |
Tarehe 4, Novemba, ujenzi wa Daraja la Bonde la Mto Huajiang la Guizhou ambalo litakuwa daraja la juu zaidi duniani umekamilisha kazi ya kufunga boriti ya kwanza ya chuma, ambapo ujenzi wa daraja hilo umeingia kipindi kipya na kuweka msingi kwa ajili ya kuzinduliwa rasmi kwa daraja hilo mwakani.
Daraja la Bonde la Mto Huajiang lililoanza ujenzi wake mwaka 2022 ni maarufu kwa sababu ya kuwa linavuka Bonde la Mto Huajiang lililosifiwa kama "ufa wa dunia". Urefu wa jumla wa Daraja hilo umefikia mita 2,980, na kimo chake kutoka juu ya usawa wa maji kimefikia mita 625. Daraja hilo litakuwa daraja la juu zaidi duniani baada ya ujenzi wake kukamilishwa.
(Tao Liang/Xinhua)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma