Lugha Nyingine
Habari Picha: Kituo cha Kiviwanda cha Shenzhen chashuhudia historia ya usambazaji na usafirishaji bidhaa kati ya Hong Kong na China Bara (3)
Kituo cha Kiviwanda cha Qingshuihe katika Eneo la Luohu, Mji wa Shenzhen wa China, hapo awali kilikuwa stesheni ya reli kwenye Reli ya Guangzhou-Kowloon. Katika miaka ya 1960, ili kuhakikisha mahitaji ya kimsingi ya maisha ya wakazi wa Hong Kong, treni maalum tatu za mizigo zilizopewa jina la “Treni Tatu za Haraka za Usambazaji Bidhaa Freshi kwa Hong Kong na Macau” (zinazojulikana kama "Treni Tatu za Haraka") zilianza kufanya kazi rasmi mwaka 1962. Hii ni stesheni ya mwisho ya reli kwa treni hizo tatu, ambayo inahusika na usafirishaji na utumaji wa bidhaa freshi.
Juni 16, 2010, kwa kukamilika kwa safari ya mwisho ya treni Na. 755, moja kati ya "Treni Tatu za Haraka", katika Stesheni ya Reli ya Zhengzhou Kaskazini, "Treni Tatu za Haraka" hizo zilimaliza kazi yake maalum ya miaka 48.
Kwa sasa imebadilishwa kuwa Kituo cha Kiviwanda cha Shenzhen na Mtaa wa Kitamaduni na Ubunifu wa Shenzhen-Hong Kong, huku kukiwa na Makumbusho maalum kwa ajili ya “Treni Tatu za Haraka”. Katika Jumba la Makumbusho la "Treni Tatu za Haraka", watembeleaji wanaweza kupitia na kujionea kumbukumbu za zama hii inayounganisha Shenzhen na Hong Kong.
Taihe, Jiangxi, China: Ujenzi wa Daraja la Chengjiang waendelea kwa kasi
Mawimbi ya Baridi Kali Yaikumba China, Maeneo Mengi Yashuhudia Kuanguka kwa Theluji
Theluji yaanguka kwa mara ya kwanza mwaka huu kwenye Milima Emei, China
Mkutano wa 19 wa Viongozi wa Kundi la 20 (G20) kufanyika Rio de Janeiro
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma