Lugha Nyingine
Tarishi mwenye kujituma sana kwenye njia ya baharini ya Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China (6)
Shi Jinquan akiwa amebeba vifurushi katika bandari ya Kijiji cha Sandu, Mji wa Ningde, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China, Desemba 2, 2024. (Picha na Feng Kaihua/ Xinhua) |
Shi Jinquan ni tarishi wa posta kwenye njia pekee ya baharini ya Mkoa wa Fujian, Kusini mwa China, ambaye anahudumia visiwa vinne, vijiji vinane na jumuiya nane za wavuvi za pwani.
Wakati akiwa na umri wa miaka 8, Shi alianza kuambatana na baba yake, ambaye ni tarishi wa zamani wa posta wa njia hiyo, kupeleka barua, na rasmi alichukua nafasi hiyo ya baba yake wakati akiwa na umri wa miaka 18. Amekuwa akihudumu hapa kwa miaka 27.
Kila siku saa 2 asubuhi, Shi huanza kuchambua na kupakia barua na vifurushi vya kupelekwa kwa watu kwa haraka katika kituo cha huduma za posta katika Kitongoji cha Sandu, kisha huendesha boti yake kuvipeleka kwa watu husika.
Ingawa visiwa hivyo viko mbali na jumuiya za wavuvi ni kama fumbo lenye kuchanganya, Shi anaweza kufikisha kwa usahihi barua na vifurushi kwa kila familia katika eneo la baharini la Sanduao kwa kutumia njia maalum za kipekee kama vile sehemu lilipo jua, mwelekeo wa mawimbi, na umbo la milima.
Sasa, amekuwa na ufahamu vema wa kila kijiji kisiwani na kila jumuiya ya wavuvi katika eneo hilo la baharini. Wavuvi na wanakijiji wanamshukuru sana.
"Baba yangu aliniambia kwamba kuchagua kazi hii inamaanisha kuchagua wajibu," amesema Shi Jinquan, "Isipokuwa wakati wa tufani, huduma ya posta kwenye njia hii haiwezi kukatizwa bila kujali jua kali la kuchoma au mvua kubwa."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma