超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Biashara ya nje ya China yaonyesha ukuaji tulivu katika miezi 11 ya kwanza?ya mwaka huu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 11, 2024
Biashara ya nje ya China yaonyesha ukuaji tulivu katika miezi 11 ya kwanza?ya mwaka huu
Malori na magari ya kazi za uhandisi yakisubiri kupakiwa kwenye Bandari ya Yantai mkoani Shandong, Mashariki mwa China, Desemba 10, 2024. (Picha na Tang Ke/Xinhua)

BEIJING –Takwimu rasmi zilizotolewa jumanne na Mamlaka Kuu ya Forodha ya China (GAC) zimeonyesha kuwa, thamani ya jumla ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa ya China imedumisha ukuaji tulivu katika miezi 11 ya kwanza ya Mwaka 2024, ikiongezeka kwa asilimia 4.9 kuliko mwaka jana wakati kama huo, ambapo thamani hiyo ya biashara ya bidhaa imeongezeka hadi yuan trilioni 39.79, sawa na dola za Kimarekani trilioni 5.6, katika kipindi cha Januari hadi Novemba.

Takwimu hizo za GAC zimeonyesha kuwa, thamani ya uuzaji nje bidhaa ya China imepanda kwa asilimia 6.7 mwaka hadi mwaka katika kipindi hicho hadi kufikia yuan trilioni 23.04, wakati uagizaji bidhaa kutoka nje umepanda asilimia 2.4 hadi kufikia yuan trilioni 16.75.

Katika Mwezi Novemba, thamani ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa iliongezeka kwa asilimia 1.2 hadi kufikia jumla ya Yuan trilioni 3.75 -- ikidumisha ukuaji kwa mwezi wa nane mfululizo.

Hasa, mauzo ya nje ya bidhaa za mitambo na umeme ya China yamechukua karibu asilimia 60 ya thamani ya jumla katika kipindi hicho cha Januari hadi Novemba, huku mauzo ya nje ya makontena, meli na pikipiki yakiongezeka kwa asilimia 108.7, 65.3 na 24.8, mtawalia.

Katika kipindi cha miezi hiyo 11 ya kwanza, mazao ya kilimo yalifikia soko pana la nchi za nje, kwani mauzo ya nje ya matunda na karanga kavu na freshi, mboga za majani na uyoga unaoliwa, na pombe na vinywaji baridi yaliongezeka kwa asilimia 22.2, 11.4 na 7.5, mtawalia.

Kampuni binafsi katika kipindi hicho zimeshuhudia biashara yao ya nje ikiongezeka kwa asilimia 8.7 mwaka hadi mwaka -- zikiendelea kuongoza biashara ya nje ya China. Wakati huo huo, uagizaji na uuzaji nje bidhaa wa kampuni zinazowekezwa na mtaji wa kigeni uliongezeka kwa asilimia 1.1.

Mwelekeo wa kugawanya soko pia uliendelea kuwa na kasi. Katika miezi hiyo 11 ya kwanza ya mwaka 2024, biashara ya China na wenzi wake wa jadi kama vile Umoja wa Ulaya, Marekani na Korea Kusini imepata ukuaji wa asilimia 1.3, asilimia 4.2 na asilimia 6.3 mtawalia.

Thamani ya biashara kati ya China na nchi zinazoshiriki katika ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja katika kipindi hicho iliongezeka kwa asilimia 6, huku ile ya nchi za ASEAN ikiongezeka kwa asilimia 8.6.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha