Lugha Nyingine
Mwelekeo wa kuimarika kwa uchumi wa China waongezeka huku kukiwa na kuendelea kutoa sera za uungaji mkono (4)
Mfanyakazi akifanya kazi kwenye karakana ya kampuni ya nguo katika Mji wa Lianyungang, Mkoani Jiangsu, mashariki mwa China, Desemba 16, 2024. (Picha na Geng Yuhe/Xinhua) |
BEIJING – Mwelekeo wa kuimarika kwa uchumi wa China umeongezeka mwezi Novemba, kutokana na kutolewa kwasera mbalimbali za kuunga mkono hivi karibuni, ambapo athari za sera hizo zimeendelea kujitokeza, na kutoa matokeo bora katika viwango muhimu vya uchumi kama vile pato la viwanda, uwekezaji, matumizi na huduma kwa mwezi huo uliopita, Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) imesema.
"Kutokana na hatua hizo za kisera, uchumi wa China umepata ukuaji tulivu kwa ujumla, huku mambo chanya yakiongezeka," msemaji wa NBS Fu Linghui amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari Jumatatu.
Msemaji huyo amesema kuwa thamani ya ongezeko ya viwanda, ambayo ni kiwango muhimu cha uchumi, iliongezeka kwa asilimia 5.4 mwaka hadi mwaka mwezi Novemba, ikionyesha ukuaji tulivu, kutokana na mpango wa kuboresha vifaa vingi na mpango wa biashara ya kubadilisha bidhaa za walaji.
Pato la sekta ya uundaji vifaa liliongezeka kwa asilimia 7.6 mwezi Novemba kuliko mwaka jana wakati kama huo, ikiwa ni asilimia 1 zaidi ya mwezi uliopita, likichukua karibu nusu ya ukuaji wa jumla wa pato la viwanda, takwimu hizo za NBS zinaonyesha.
Kiwango cha wasimamizi wa ununuzi katika sekta ya viwanda ilifikia 50.3 mwezi uliopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 0.2 kutoka mwezi uliopita na kupita ile ya 50 kwa mara ya pili tangu iliporejea kuongezeka kwake Oktoba baada ya miezi mitano mfululizo ya kupungua.
Fu amezungumzia pia kuongezeka kwa mahitaji katika suala la uwekezaji na matumizi. Uwekezaji wa rasilimali zisizohamishika nchini China uliongezeka kwa asilimia 3.3 mwaka hadi mwaka katika miezi 11 ya kwanza ya 2024, ikiwa ni ongezeko la yuan trilioni 46.5839 (dola za Marekani kama trilioni 6.48).
Mwezi Novemba, mauzo ya rejareja ya bidhaa za walaji nchini China yalipanda kwa asilimia 3 mwaka hadi mwaka na kufikia Yuan trilioni 4.38 mwezi Novemba, Fu amesema.
Msemaji huyo pia amesema kuwa ubora wa ukuaji wa uchumi wa China unaendelea kuimarika. Hata hivyo, amesema kuwa mazingira ya kimataifa bado ni magumu na yenye changamoto.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma