Treni zinazosafiri kati ya China na nchi za nje, shughuli za biashara zenye pilikapilika, na bidhaa za aina mbalimbali.
Kwa Mji wa Guiyang katika Mkoa wa Guizhou, China wakati wa usiku, pilikapilika ni jambo lisiloepukika, huku kukiwa na mabanda mengi yenye vyakula vya kienyeji vya aina mbalimbali,maduka mapya ya vyakula,maduka madogo na yenye kupendeza ya vitu vya kitamaduni na kibunifu,,,yakileta pilika nyingi kote mtaani. Sehemu kubwa ya maisha ya usiku ya watu wa Guiyang huanza na vitafunwa vya usiku.
Maonesho ya ustadi wa kupanda farasi. (Picha na Li Long/People’s Daily Online) Wakati tu ambapo Mkoa wa Xinjiang, China unaingia kwenye msimu wake wa pilikapilika za utalii za mwezi Juni, Bustani ya Kale ya Farasi Pori ya Xinjiang (kwa ufupi inajulikana kama Farasi Pori) iliyopo Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo imevutia ufuatiliaji wa watu wengi mtandaoni.
Wakati usiku unapoanza na taa kuwashwa, gulio kubwa la kimataifa la mkoani Xinjiang, China hujaa watu wengi na kuonesha hali motomoto. Kwenye Mtaa wa chakula wa Gulio Kubwa la Kimataifa la Xinjiang, China ukiwa umezungukwa na taa nzuri za mapambo, sauti za nyimbo za jadi za kabila la Wauygur zinasikika eneo zima, salamu za makaribisho ya wauzaji na mazungumzo ya wateja ni kila mahali, na nyama choma ya mbuzi, kuku pilipili na vyakula vingine mbalimbali vinaonesha picha ya maisha ya usiku ya mji yenye hali motomoto, yakivutia watalii wengi kutoka ndani na nje ya China kwenda huko kutembelea soko hilo la usiku, kuonja chakula kitamu na kujionea uzuri wa Xinjiang.