Lugha Nyingine
Benki Kuu ya Afghanistan kuingiza dola milioni 12 sokoni ili kuleta utulivu katika sarafu ya nchi hiyo
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 20, 2022
KABUL - Benki Kuu ya Afghanistan, Benki ya Da Afghanistan (DAB), imesema Jumapili kuwa itaingiza zaidi dola za Kimarekani milioni 12 katika soko la ndani ili kukuza sarafu ya nchi hiyo.
DAB imesema katika taarifa yake kwamba inazitaka benki zote zinazostahiki na watoa huduma za kifedha kushiriki katika mnada uliopangwa kufanyika leo Jumatatu.
"Katika zabuni za mnada, hairuhusiwi kulipa kwa sehemu ya malipo na washindi wa mnada lazima waweke malipo yao yote ya fedha taslimu katika Benki ya Da Afghanistan kwa wakati mmoja," imesema taarifa hiyo.
Dola ya Marekani imeshuka thamani dhidi ya sarafu ya Afghanistan ikilinganishwa na wiki chache zilizopita. DAB ilifanya mnada wa dola milioni 11 mapema wiki hii.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma