Lugha Nyingine
Watu wateleza kwenye mawimbi na kufurahia mandhari nzuri ya Wanning, Hainan (7)
Katika Ghuba ya Riyue ya Wanning mkoani Hainan, watalii wanateleza kwenye mawimbi baharini na kufurahia wakati mzuri wa majira ya joto. Katika miaka ya hivi karibuni, michezo ya kuteleza kwenye mawimbi imeenea sana, na watalii wengi zaidi wanakuja Wanning, Hainan ili kujifunza michezo hiyo na kujiburudisha kwa furaha kwenye bahari.
Kutokana na hali nzuri ya kijiografia na ya hali ya hewa, michezo ya kuteleza kwenye mawimbi baharini imekuwa kivutio kwenye utalii wa Wanning. Wanavijiji wengi wameanza kufanya biashara katika utoaji mafunzo ya kuteleza kwenye mawimbi baharini, kuendesha migahawa na hoteli, na wamepata manufaa kutokana na maendeleo ya shughuli zao.
Bustani ya Wanyama ya Chongqing yawasaidia wanyama kuepuka joto
Watu wafuruhia hali ya hewa nzuri wakati wa majira ya joto kwenye sehemu ya Mto Wujiang, Chongqing
Bwawa la Sanmenxia la katikati mwa China laanza kufanya kazi ya Kuondoa tope la mchanga
Mandhari ya Ziwa Yamdrok katika Mji wa Shannan, Mkoa wa Tibet, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma