Lugha Nyingine
Habari Picha: Mandhari nzuri ya kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo baharini cha Daraja la Donghai,Shanghai
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 17, 2023
Tarehe 15, Februari, mandhari ya kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo baharini cha Daraja la Donghai katika mji wa Shanghai wa China, ilikuwa nzuri sana pamoja na anga ya buluu na mawingu meupe.
Kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo baharini cha Daraja la Donghai kinapatikana katika pande zote mbili za Daraja la Donghai, kutoka mji mpya wa Lingang, katika Pudong, eneo jipya la Shanghai, hadi Bandari ya Maji ya Kina ya Yangshan. Kituo hicho si tu ni mradi wa kwanza wa mfano wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo baharini nchini China, bali pia ni kituo kikubwa cha kwanza cha kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo baharini barani Asia. (Picha na Wangchu)
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma