Lugha Nyingine
Habari Picha: Magari yakionyeshwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Tasnia ya Magari ya Shanghai 2023
Gari la Kampuni ya Magari ya Volkswagen modeli ya SAIC Volkswagen ID.6 X likionyeshwa kwenye Maonyesho ya 20 ya Kimataifa ya Tasnia ya Magari ya Shanghai huko Shanghai, Mashariki mwa China, Aprili 24, 2023. (Xinhua/Fang Zhe)
Watengenezaji magari duniani wanashindana kuonyesha bidhaa zao bora mpya za magari yanayotumia nishati mpya kwenye Maonyesho ya Magari ya Shanghai 2023 yanayoendelea, na kuakisi juhudi zao za kupata sehemu ya soko la magari yanayotumia nishati mya (NEVs) la China huku kukiwa na ushindani mkali.
Mratibu wa maonyesho hayo amesema kuwa karibu magari 1,500 yanaonyeshwa kwenye maonyesho hayo, na magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) yanachukua zaidi ya nusu ya magari hayo. Maonyesho hayo, kutawaliwa na NEVs, pia kunaonyesha mwelekeo wa kiteknolojia katika soko la kimataifa la magari.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma