Lugha Nyingine
Mashariki ya Kati kwenye Picha: Kundi la wasanii wa China kufanya maonesho wakati wa Tamasha la kimataifa la Carthage nchini Tunisia
TUNIS, Agosti 10 (Xinhua) -- Tamasha la 57 la Kimataifa la Carthage linafanyika katika kituo cha Carthage katika Tunis, mji mkuu wa Tunisia. Wacheza ngoma kutoka kundi la wasanii la Ningxia la China wameshiriki kwenye tamasha hilo kwa kufanya maonyesho mazuri kwa ajili ya watazamaji.
Kituo cha Carthage kilichojengwa katika karne ya 9 K.K., ni kituo cha Urithi wa Dunia kilichowekwa kwenye orodha ya UNESCO na moja ya maeneo maarufu ya utalii. Tamasha hilo linalofanyika kila majira ya joto wakati wa msimu wa watalii, ni tamasha kubwa zaidi la michezo ya sanaa lenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Tunisia, huku wasanii kutoka nchi mbalimbali duniani wakifanya maonesho ya michezo ya Sanaa katika ukumbi wa michezo wa kale wa Kirumi kwenye kituo hicho.
Kituo hicho kilifunguliwa tena mwaka jana baada ya kusimama kwa miaka miwili kutokana na janga la COVID-19. Tamasha la mwaka huu lilianza Julai 14 na litafanyika hadi Agosti 19.
Habari ya Picha: Mandhari Nzuri ya Mbuga ya Milimani huko Yunnan, China
Wakulima washughulikia kuvuna mazao ya mbegu za mayungiyungi huko Wilaya ya Quannan, Mkoa wa Jiangxi
Panda "Ruyi" na "Dingding" washerehekea siku ya kuzaliwa huko Moscow
Safari isiyoweza kusahaulika ya mcheza dansi wa Russia katika Mkoa wa Xinjiang, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma