Lugha Nyingine
Rais Xi na mwenzake wa Uruguay Lacalle wafanya mazungumzo, wainua uhusiano wa pande mbili kuwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo na Rais wa Uruguay Luis Alberto Lacalle Pou mjini Beijing siku ya Jumatano ambapo wakuu hao wawili wa nchi wametangaza kuinua uhusiano wa pande mbili hadi kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote.
Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Uruguay, na ni mwaka wa tano tangu Uruguay ijiunge na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, Rais Xi amesema tangu kuanzishwa kwa uhusiano huo wa kidiplomasia, nchi hizo mbili zimetilia maanani kuheshimiana, kutendeana kwa usawa na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.
“China iko tayari kufanya kazi na Uruguay kutumia fursa ya kuanzishwa kwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande zote kama mwanzo mpya na hatua mpya ya kuinua kiwango cha uhusiano wa nchi hizo mbili na kuongeza mambo ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kuufanya uhusiano kati ya China na Uruguay kuwa mfano wa mshikamano na ushirikiano kati ya nchi zenye tofauti katika ukubwa, mifumo na tamaduni, ili utumikie vyema maendeleo ya nchi hizo mbili, na kuboresha ustawi wa watu wa pande hizo mbili” amesema Rais Xi.
Amefafanua kuhusu maana na umuhimu wa maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, akisema kuwa China iko tayari kuimarisha hali ya kubadilishana mawazo na Uruguay kuhusu utawala wa nchi, kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kuchangia fursa za maendeleo, na kuhimiza maendeleo ya mambo ya kisasa ya nchi hizo mbili na Dunia.
Ametoa wito kwa pande hizo mbili kuzidisha mawasiliano ya kirafiki na ushirikiano kati ya mabunge, vyama vya siasa na serikali za mitaa; kuchukua utiaji saini wa mpango wa ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja kama fursa ya kuimarisha muunganisho wa mikakati ya maendeleo; kuhamasisha vichocheo vipya vya ushirikiano katika biashara ya huduma, uchumi wa kidijitali na nishati safi; na kusukuma ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja wa China na Uruguay kwenye hatua mpya ya maendeleo yenye ubora wa hali ya juu.
Kwa upande wake Lacalle amesema kuwa serikali ya Uruguay inatambua kuwa kuna China moja tu duniani, na kwamba Muungano wa amani ni jambo la ndani la China na lazima liamuliwe na watu wa China wenyewe.
“Uruguay na China zinalinda kithabiti ushirikiano wa pande nyingi na biashara huria, na zimejitolea kuhimiza amani na utulivu duniani,” amesema, huku akisisitiza kuwa uhusiano wa Uruguay na China umevuka sekta za uchumi na biashara, na umeonyesha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya pande nyingi na kwenye kiwango cha juu .
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma