Lugha Nyingine
Chombo?cha AS700?cha kuendeshwa angani cha China chakamilisha safari kielelezo ya kuruka anga ya chini (3)
Chombo cha AS700 cha kuendeshwa angani kikifanya safari kielelezo ya kuruka angani huko Jingmen, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Agosti 1, 2024. ( Kampuni ya Kundi la Viwanda vya Usafiri wa Angani la China/kupitia Xinhua) |
HUBEI - Utalii kwenye anga ya chini nchini China unaingia katika njia mpya wakati ambapo chombo cha AS700 cha kuendeshwa angani chenye umbo la puto kilichoundwa nchini China kimefanikiwa kufanya safari yake ya kwanza ya kielelezo siku ya Alhamisi asubuhi, ambapo chombo hicho kilipaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Zhanghe huko Jingmen, Mkoa wa Hubei wa China, kuonyesha ufanisi na uwezo wake katika kuhudumia utalii kwenye mbingu.
Safari hiyo kielelezo ya chombo hicho ilidumu kwa saa takriban mbili, ikiiga mazingira mbalimbali ya kufanya utalii kwenye mbingu kupitia njia iliyopangwa.
Chombo hicho kiliruka juu ya bustani za mji huo, kisiwa kilicho kwenye mto na maeneo mengine maarufu ya vivutio vya utalii katika mji mzima na kisha kurudi salama. Kilikuwa kikiendeshwa kwa kasi ya kilomita 60 kwa saa na urefu wa mita 500 kutoka usawa wa kiwango fulani kwenye ardhi wakati wa safari hiyo, limesema Kampuni ya Kundi la Viwanda vya Usafiri wa Angani la China (AVIC).
Kwenye mbingu, abiria waliopanda chombo hicho cha AS700 wanaweza kufurahia hali ya kupendeza ya angani kupitia madirisha makubwa ya pembeni ya kipanoroma. Kwa wastani wa kasi yake inayofaa na urefu unaofaa kutoka usawa wa kiwango fulani kwenye ardhi kwa kutazama hali ya maeneo ya mbingu, chombo hicho kitawapa watalii uzoefu kama "kuelea juu ya mawingu" wakati wa safari tulivu na salama ya chombo hicho, Kampuni ya AVIC, imesema.
Kikiwa kimeundwa na Taasisi ya Utafiti wa Vyombo Maalum ya AVIC, AS700 ni chombo cha kuruka angani chenye sehemu moja ya kubeba watu, ambacho kina uwezo wa juu zaidi wa kubeba watu 10, akiwemo rubani. Kina uzito wa juu wa kupaa angani wa kilo 4,150, ukomo wa kuruka wa umbali wa kilomita 700, na uhimilivu wa juu wa kuendeshwa kwa saa 10, AVIC limesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma