Lugha Nyingine
Askari wa zamani wa Japan wa kikosi cha vita vya kutumia vijidudu afichua uhalifu wa kivita nchini China
HARBIN - Hideo Shimizu, askari wa zamani wa Kikosi cha 731 cha jeshi la Japan ambacho ni kikosi hatari cha vita vya kutumia vijidudu cha Japan wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, amebainisha uhalifu wa Jeshi la Japan siku ya Jumanne katika eneo alilofanya kazi wakati wa vita hivyo miaka 79 iliyopita nchini China.
Shimizu mwenye umri wa miaka 94, ni miongoni mwa kundi la mwisho la Askari Vijana wa Kikosi cha 731 waliotumwa na Japan kwenda Harbin, China, ambako alitumia zaidi ya miezi minne kushuhudia uhalifu wa kivita uliokuwa ukifanywa na kitengo hicho, ikiwa ni pamoja na ukuzaji wa vimelea vya magonjwa, upasuaji wa binadamu na majaribio ya binadamu. Alitoroka China na vikosi vya Japan vilivyokuwa vikirudi nyuma mnamo Agosti 14, 1945.
Ziara hii ni ya kwanza kwa Shimizu kurejea katika ardhi ya China katika miaka 79 iliyopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma