Lugha Nyingine
Ukingo wa lambo uliobomoka katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani wazibwa (9)
Picha ya droni iliyopigwa Agosti 14, 2024 ikionyesha waokoaji wakifanya kazi kwenye eneo la ukingo wa lambo uliobomoka katika Kitongoji cha Taipingdi cha Mji wa Chifeng, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China. (Xinhua/Bei He) |
HOHHOT – Ukingo wa lambo uliobomoka kwenye mto ulio Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China ulikuwa umezibwa kufikia saa 8:13 mchana siku ya Jumatano, na bila kusababisha vifo na majeruhi ya watu, kwa mujibu wa idara ya kinga na udhibiti wa ukame na mafuriko ya mkoa huo.
Kubomoka kwa ukingo huo wa lambo, kwenye eneo lenye urefu wa mita 10 kwa upana, kulitokea majira ya saa 6:40 mchana siku ya Jumanne kwenye Mto Laoha katika Kitongoji cha Taipingdi cha Mji wa Chifeng, kukilazimu zaidi ya wakazi 800 kuondoka kwenye makazi yao na kuathiri mashamba ya kilimo yenye ukubwa wa hekta 600.
Waokoaji zaidi ya 800 kutoka jeshi la polisi, jeshi la zimamoto, idara za usalama wa umma, idara za usimamizi wa dharura na idara zingine walitumwa kuziba ubomokaji huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma