Lugha Nyingine
China yaongeza mwitikio wa dharura kwa kimbunga Yagi katika Mikoa ya Guangdong na Hainan hadi Ngazi ya Pili (8)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 06, 2024
Picha iliyopigwa na droni Septemba 5, 2024 ikionyesha meli za wavuvi zikiwa zimetia nanga kwenye bandari ya Tanmen huko Qionghai, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China. (Picha na Meng Zhongde/Xinhua) |
BEIJING - Idara Kuu ya Kudhibiti Mafuriko na kupambana na Ukame ya China yameongeza mwitikio wake wa dharura wa kuzuia mafuriko na kimbunga kutoka ngazi ya tatu hadi ngazi ya pili katika mikoa ya Guangdong na Hainan saa 9 alasiri siku ya Alhamisi, wakati ambapo Kimbunga Yagi kinakaribia.
Kiini cha Yagi, kimbunga cha 11 kwa mwaka huu kuikumba China, kilikuwa kikionekana baharini umbali wa takriban kilomita 540 kusini mashariki mwa Wilaya ya Xuwen, Mkoa wa Guangdong, saa 8 mchana siku ya Alhamisi.
Kimbunga Yagi kinakadiria kutua Ijumaa alasiri au jioni mahali fulani kati ya mji wa Qionghai huko Hainan na Mji wa Maoming huko Guangdong.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma