Lugha Nyingine
Habari picha: Wahifadhi wajitolea kulinda hifadhi ya mazingira ya asili katika Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China
Wang Kedong na Gao Kaiyu, wote wenye umri wa miaka 58, ni walinzi na wahifadhi wa kituo cha usimamizi cha Tiantangzhai cha Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Anhui Tianma nchini China. Wanaishi milimani mwaka mzima na wamekuwa wakishika doria kila siku kwenye njia yenye urefu wa zaidi ya kilomita 20 kwa miaka 25.
Hifadhi ya Taifa ya Mazingira ya Asili ya Anhui Tianma nchini China ilianzishwa Mwaka 1998 ikiwa katika msingi wa hifadhi mbili za zamani za Mkoa wa Anhui. Iko kwenye eneo la mpito kutoka eneo la nusu tropiki hadi eneo la joto vuguvugu ikiwa na rasilimali nyingi za wanyama na mimea. Kwa vile viumbe wengi adimu na walio hatarini kutoweka wanaishi hapa, kazi ya uhifadhi na ulinzi katika hifadhi hii ni muhimu sana.
Doria na ulinzi wa misitu ni kazi ya kila siku ya wanandoa hawa wawili. Wang amesema, kuna njia saba za doria za kila siku kwa wanandoa hao, na njia ndefu zaidi ni yenye urefu wa zaidi ya kilomita 30 kwenda na kurudi, ambayo inachukua zaidi ya masaa 10 kukamilika. Kwa kukadiria kwa haraka, wawili hao wameshavaa na kuchakaza karibu jozi 1,000 za viatu na kushika doria kwenye eneo lenye urefu wa zaidi ya kilomita 200,000 katika miaka 25 iliyopita. Chini ya ulinzi na uhifadhi wao, kumekuwa hakuna ukataji miti ovyo na ujangili wa wanyama pori katika hifadhi hiyo kwa miaka mingi.
"Tuna hisia za kina kwa mlima. Ilimradi tu tunaweza kutembea, tutalinda milima hii na misitu hii kila wakati." Wang na mkewe wamesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma